Nemobase
5 min readFeb 21, 2024

Kufungua mgahawa ni ndoto ya wengi lakini inahitaji mipango thabiti, utafiti, kujituma na uvumilivu.

Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine, ina soko linalokua la migahawa, lililo na fursa nyingi za kibiashara. Hapa chini ni muongozo wa jinsi ya kufungua na kukuza mgahawa wako nchini Tanzania, kwa kutumia teknolojia na mikakati mingine muhimu.

Hatua za Kufungua Mgahawa

1. Utafiti na Mipango:
- Fanya utafiti wa soko kujua mahitaji ya wateja, ushindani, na mahali pazuri pakufanyia biashara.
- Andaa mpango wa biashara unaoelezea malengo, bajeti, mpango wa menu, na mikakati ya masoko.

Hii itakusaidia kujua biashara yako itakuaje na kujiandaa na lolote linaloweza kuipata biashara yako mbeleni. Na kumbuka tu, sio kila mpango utaenda sawa.

2. Usajili na Leseni:
- Hakikisha mgahawa wako unakidhi viwango vya usalama na afya vilivyowekwa na serikali ya Tanzania.
- Sajili jina la biashara na upate leseni ya biashara kutoka mamlaka husika.

Tanzania, leseni ya biashara inayohitajika kwa mgahawa inategemea ukubwa na aina ya mgahawa.

Mgahawa mdogo , kama vile mgahawa wa kahawa au mgahawa wa chakula cha mchana, kwa kawaida utahitaji leseni ya biashara ya kawaida kutoka kwa serikali ya mtaa. Leseni hii kwa kawaida huwa na gharama ya TZS 25,000 hadi 50,000 kwa mwaka.

Migahawa mikubwa, kama vile vile vile migahawa ya kulia chakula cha jioni na migahawa yenye leseni ya pombe, itahitaji leseni ya biashara ya aina maalum kutoka kwa Wizara ya Biashara na Viwanda. Leseni hii kwa kawaida huwa na gharama ya TZS 100,000 hadi 200,000 kwa mwaka.

Mbali na leseni ya biashara, migahawa yote nchini Tanzania inatakiwa kupata vibali vifuatavyo:

  • Cheti cha Usalama wa Chakula kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
  • Leseni ya Afya ya Umma kutoka kwa Halmashauri ya Mtaa.
  • Leseni ya Moto kutoka kwa Idara ya Zimamoto.

Gharama ya vibali hivi hutofautiana kulingana na ukubwa na aina ya mgahawa.

Hizi hapa ni baadhi ya nyaraka zinazohitajika kuomba leseni ya biashara ya mgahawa nchini Tanzania:

  • Fomu ya maombi ya leseni ya biashara iliyojazwa
  • Nakala ya cheti cha usajili wa biashara
  • Nakala ya cheti cha usalama wa chakula
  • Nakala ya leseni ya afya ya umma
  • Nakala ya leseni ya moto Risiti ya malipo ya ada ya leseni

Maombi ya leseni ya biashara yanaweza kuwasilishwa kwa serikali ya mtaa au Wizara ya Biashara na Viwanda.

Mchakato wa kupata leseni ya biashara ya mgahawa nchini Tanzania unaweza kuchukua muda wa wiki kadhaa hadi miezi kadhaa. Inashauriwa kuanza mchakato mapema iwezekanavyo.

3. Mpangilio wa Fedha:
- Tathmini gharama za mwanzo na za uendeshaji. Hii inajumuisha kodi, mishahara, gharama za chakula, na zinginezo.
- Fikiria vyanzo vya mtaji, kama vile mikopo ya benki, wawekezaji, au akiba binafsi.

Makadirio ya gharama:

  • Kodi ya Pango: TZS 50,000 - 500,000+ kwa mwezi
  • Ukarabati na Ujenzi: TZS 1,000,000 - 10,000,000+
  • Vifaa vya Jikoni: TZS 200,000 - 5,000,000+ Samani na
  • Vifaa vya Kulia: TZS 100,000 - 2,000,000+
  • Leseni: TZS 25,000 - 50,000+ kwa mwaka
  • Mshahara wa Wafanyakazi: Kinategemea ukubwa na idadi ya wafanyakazi
  • Mtaji wa Uendeshaji: TZS 500,000 - 2,000,000+ kwa mwezi
  • Jumla: TZS 3,000,000 - 20,000,000+

Malipo na Kodi:

  • Kodi ya Mapato: 10% - 30%
  • VAT: 18%
  • Kodi ya Tozo la Huduma: 10%
  • Leseni na Udhibiti wa Chakula: Ada za kila mwaka

Fanya utafiti zaidi kufahamu kiasi cha mtaji utakachokihitaji.

Kukuza Mgahawa Mtandaoni na Kutumia Teknolojia

1. Tovuti na Mitandao ya Kijamii:
 — Tumia mitandao ya kijamii (kama Instagram, Tiktok, Facebook, na Twitter) kushiriki picha za vyakula, ofa maalum, na tukio lolote linalojiri mgahawani.

— Post kila mara na jibu wateja wako wanapokuuliza maswali.

2. Programu za Utoaji Chakula:
- Jiunge na programu za utoaji chakula kama Piki, dukadirect, Glovo, au nyengine unazo zifahamu.
- Hii itasaidia kufikia wateja zaidi na kuongeza mauzo.

3. Teknolojia ya Usimamizi:
- Tumia app ya nemobase kwa ufanisi wa kusimamia mauzo, wafanyakazi, hesabu, madeni na mapato. Pia hivi karibuni utaweza kupokea malipo, kutunza fedha n.k
- Fikiria kutumia programu za usimamizi wa wateja kuboresha huduma na kujenga uaminifu.

Unaweza kupakua app ya nemobase kupitia linktr.ee/nemobase au App store na Playstore.

Ukiwa na maswali zaidi unaweza kuwasaliana nasi kupitia Whatsapp kwa kubonyeza hapa.

Delivery ya Chakula cha Mgahawa wako.

Delivery ni huduma muhimu kwa mgahawa wowote hivi sasa Tanzania. Kufanikisha mfumo bora wa delivery ya chakula cha mgahawa wako, zingatia mambo yafuatayo:

1. Chagua Mbinu ya Delivery:

Ya ndani: Ajiri madereva wa pikipiki au magari.

Ya Nje: Tumia kampuni ya delivery kama vile Piki au Duka.direct

2. Teknolojia:

Tumia programu ya simu ya kupokea maagizo na kufuatilia maendeleo ya delivery. Au unaweza kuboresha mawasiliano yako kwa kutumia WhatsApp.

3. Ubora wa Chakula:

Hakikisha chakula kinafika moto na safi kwa mteja. Tumia vifungashio vinavyofaa na vinavyoweza kutunza ubora wa chakula.

4. Huduma kwa Wateja:

Kuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano na wateja. Waambie wateja kuhusu hali ya delivery zao. Kuwa na mfumo wa kushughulikia malalamiko ya wateja.

5. Gharama na Faida:

Hesabu gharama za delivery na uhakikishe bei zinafaa. Toa ofa za kuvutia wateja kama vile punguzo la delivery au chakula cha bure.

6. Uuzaji na Tangazo:

Tangaza huduma ya delivery kwenye mitandao ya kijamii, tovuti yako, na kwenye vipeperushi. Shiriki katika matukio ya chakula na utoe sampuli za chakula chako.

Hakikisha madereva wako wamevaa mavazi rasmi na wana tabia njema. Weka viwango vya juu vya usafi na usalama wa chakula. Pata leseni na vibali vyote vinavyohitajika kwa ajili ya delivery ya chakula. Fuatilia maoni ya wateja na fanya maboresho mara kwa mara.

Kwa kufuata miongozo hii, unaweza kuhakikisha mfumo bora wa delivery ya chakula cha mgahawa wako nchini Tanzania na kuvutia wateja zaidi.

Safari ya Anitha Kufungua Mgahawa

Anitha akiwa katika mgahawa wake

Anitha alitamani kufungua mgahawa wake tangu alipokuwa mdogo. Baada ya kufanya utafiti wa kina na kuandaa mpango wa biashara, alipata mkopo kutoka benki na kufungua mgahawa wa vyakula vya asili wa "Taste of Tanzania" katikati ya Dar es Salaam.

Anitha alitumia mitandao ya kijamii kujenga uwepo mtandaoni hata kabla ya mgahawa kufunguliwa, aki post hadithi za vyakula vyake na utamaduni wa Kitanzania.

Alitumia app ya nemobase kusimamia mauzo na hesabu, na kujiunga na programu ya utoaji na usambazaji chakula ili kufikia wateja wengi zaidi. Kupitia kujituma, huduma bora, na kutumia teknolojia, "Taste of Tanzania" ilikua na kupata umaarufu, huku Anitha akipanga kupanua biashara yake kwa kufungua matawi mengine.

Kufungua na kukuza mgahawa Tanzania inahitaji mipango, bidii, na matumizi ya teknolojia ya kisasa. Kwa kufuata hatua hizi, na kuhamasishwa na hadithi kama ya Anitha, unaweza kufikia mafanikio katika sekta ya migahawa.

Nemobase
Nemobase

Written by Nemobase

Kuwa mjasiriamali wa kizazi kipya 💙

No responses yet