Hongera kwa kufanikiwa kujiandikisha kwenye app ya Nemobase! Kwa kutumia app hii, utaweza kusimamia bidhaa na huduma zako kwa urahisi na ufanisi. Fuata mwongozo huu wa hatua kwa hatua ili kuanza kutumia app ya Nemobase.
Baada ya kujiandikisha, hatua ya kwanza ni kuingiza bidhaa zako katika katalogi.
Fuata hatua hizi:
a. Bonyeza kwenye kichupo au kitufe kinachosema "Ongeza bidhaa".
b. Jaza taarifa zifuatazo kuhusu kila bidhaa:
- Jina la bidhaa: Andika jina la bidhaa.
- Maelezo: Toa maelezo kuhusu bidhaa, hasa ikiwa mtu mwingine tofauti na mmiliki atakuwa anaishughulikia.
- Upakiaji: Eleza aina ya ujazo au upakiaji wa bidhaa, kama vile KG, chupa, n.k.
c. Tumia kitufe cha kubadili (toggle) kwa bidhaa zisizohesabika kama nafaka, sukari, maziwa, n.k.
- Weka "Bidhaa ni ya kuhesabika" kuwa ON ikiwa bidhaa inaweza kuhesabiwa.
- Weka kuwa OFF ikiwa bidhaa haiwezi kuhesabiwa.
d. Andika idadi ya bidhaa zilizopo kwenye hesabu yako katika sehemu ya Idadi.
e. Kiasi cha chini cha kutoa tahadhari: Weka idadi ndogo ya bidhaa ambayo app itakukumbusha kuongeza hesabu.
f. Kama hujui bei ya kununulia, zima kitufe cha "Jaza bei ya kununulia".
- Bei ya kununulia: Andika bei ambayo ulinunua bidhaa.
- Bei ya kkuuzia Andika bei unayotarajia kuuza bidhaa.
g. Bonyeza "Tunza bidhaa" kuhifadhi taarifa zilizoingizwa.
Ikiwa biashara yako inahusisha huduma badala ya bidhaa za kimwili, fuata hatua hizi:
a. Nenda kwenye kichupo cha bidhaa kisha bonyeza kitufe cha "+".
b. Bonyeza "Ongeza huduma".
c. Jaza taarifa zifuatazo kuhusu kila huduma:
- Jina la huduma: Andika jina la huduma, kama vile "Kunyoa na black", "Kunyoa mtoto", "Scrub", n.k.
- Maelezo: Toa maelezo kuhusu huduma.
- Bei: Weka bei ya huduma hiyo.
d. Bonyeza "Wasilisha" kuhifadhi huduma uliyoongeza.
Kwa kuongeza mauzo kupitia app ya Nemobase, fuata hatua zifuatazo:
a. Anza Kwa Kufungua Oda Mpya:
- Bonyeza "Ongeza oda" ili kuanza kuingiza taarifa za mauzo mapya.
b. Ongeza Taarifa za Mteja:
- Ongeza mteja: Jaza jina na namba ya simu ya mteja wako ili kuwa na kumbukumbu za mawasiliano.
c. Chagua Bidhaa na Huduma:
- Chagua bidhaa: Ongeza bidhaa zilizonunuliwa kwa kubonyeza sehemu imeandikwa Ongeza bidhaa. Unaweza kuchagua bidhaa na huduma kwa wakati mmoja. Tumia kitufe cha '+' kuongeza idadi ya bidhaa au '-' kupunguza.
d. Weka Punguzo (Discount):
- Jumla ya punguzo: Andika kiwango cha punguzo ulichompa mteja, kama kipo.
e. Gharama ya Usafirishaji:
- Gharama ya usafirishaji: Weka kiasi cha ada ya usafirishaji, endapo bidhaa zinahitaji kutumwa.
f. Toa Maelezo ya Kodi:
- Kodi: Ingiza kiasi cha kodi kinachohitajika kama unaweza kukadiria.
g. Udhibiti wa Malipo ya Deni:
- Kama mauzo ni ya deni, weka kwenye hali ya "imelipwa kidogo" na andika kiasi kilicholipwa kwenye "Kiasi kilicholipwa". Hii itasaidia kufuatilia madeni kwa urahisi.
h. Badilisha Tarehe ya Mauzo:
- Kama mauzo hayakufanyika siku hiyo, unaweza kubadili tarehe kwa kubofya kwenye tarehe iliyoonyeshwa chini na kuiweka tarehe sahihi ya mauzo.
i. Hifadhi Taarifa za Mauzo:
- Bonyeza "Tunza mauzo" ili kuhifadhi taarifa zote za mauzo uliyoingiza.
Kwa kutumia hatua hizi, utaweza kusimamia mauzo yako kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha kwamba taarifa zote zinabaki kuwa sahihi na za kisasa. Endelea kutumia Nemobase kwa urahisi na ufanisi wa hali ya juu katika biashara yako.
Kudhibiti matumizi yako kupitia app ya Nemobase ni rahisi. Fuata hatua zifuatazo:
a. Anza Kwa Kufungua Kipengele cha Matumizi:
- Bonyeza kitufe kinachosema "Rekodi matumizi" ili kuanza kuingiza matumizi mapya.
b. Ingiza Taarifa za Matumizi:
- Kiasi: Andika kiasi cha fedha kilichotumika.
- Maelezo: Eleza aina ya matumizi, kama vile chakula, vinywaji, umeme, n.k.
- Tarehe ya matumizi: Weka tarehe ambayo matumizi yalifanyika, endapo siyo ya siku hiyo.
c. Hifadhi Taarifa za Matumizi:
- Bonyeza "wasilisha" ili kuhifadhi taarifa za matumizi uliyoingiza.
1. Tazama Ripoti ya Biashara:
- Bonyeza "Ona zaidi" pembeni ya uchambuzi wa mauzo ya leo kuangalia ripoti ya biashara ya muda wote.
2. Angalia Bidhaa na Huduma Zako:
- Bonyeza "Bidhaa" kwa chini kuona orodha ya bidhaa na huduma zako.
3. Review Mauzo na Matumizi:
- Bonyeza "Mauzo" kwa chini kuangalia mauzo na matumizi yako yote.
4. Mipangilio ya Akaunti:
- Bonyeza "English" au "Kiswahili" kubadili lugha ya app.
- Bonyeza "Sasisha profile" ku-edit profaili yako.
- Bonyeza "Badili neno la siri" kubadilisha neno la siri lako.
- Bonyeza "Manage staff" kuongeza au kusimamia wafanyakazi na kudhibiti ufikiaji wao kwenye akaunti yako.
- Bonyeza "Msaada" kuchati nasi kwa WhatsApp kwa msaada zaidi.
- Bonyeza "Ondoka" kutoka nje ya app.
Kumbuka:
Endelea kufuatilia akaunti zetu za mitandao ya kijamii au YouTube kupitia jina: @nemobase kwa taarifa zaidi na mafunzo kuhusu app ya Nemobase. Unaweza kuchati nasi kupitia WhatsApp ikiwa unahitaji msaada zaidi wakati wowote.