Bi. Amina ni mfanyabiashara mwenye duka la vifaa vya umeme mjini Dar es Salaam. Katika duka lake, Bi. Amina anauza vifaa kwa bei tofauti, lakini wateja wake wengi wanashindwa kumudu kulipia gharama ya vifaa hivyo kwa mara moja.
Ili kuwasaidia wateja wake, Bi. Amina aliamua kutumia app ya Nemobase kurekodi mauzo yanayolipiwa mdogo mdogo.
Kupitia Nemobase, Bi. Amina anawawezesha wateja wake kununua vifaa kwa awamu ndogo ndogo, na hivyo kuongeza mauzo yake na kuboresha uhusiano na wateja. Bi. Amina amegundua kuwa kwa kutumia mfumo huu, wateja wake wanakuwa waaminifu zaidi na wanarudi tena kununua bidhaa nyingine.
Faida za kuuza vitu kwa malipo mdogo mdogo.
Naamini umeshaona wauzaji wengi wa vifaa vya umeme, urembo n.k. wamekua wakipokea malipo mdogo mdogo ya bidhaa zao. Unahisi kwanini? Hizi ndizo sababu:
1. Kupunguza Mzigo wa Malipo: Malipo mdogo mdogo yanawezesha wateja kulipia bidhaa au huduma kwa awamu ndogo ndogo. Hii inapunguza mzigo wa kulipia kwa mara moja, na kuwafanya wateja waweze kumudu gharama kwa urahisi zaidi.
2. Kuongeza Uaminifu: Kwa kuruhusu malipo kwa awamu, wafanyabiashara wanaweza kujenga uaminifu na wateja wao. Wateja wanajisikia salama kununua bidhaa kwa sababu wana uhakika wa kumudu gharama hizo polepole.
3. Kuongeza Mauzo: Mfumo wa malipo mdogo mdogo huongeza idadi ya wateja wanaoweza kumudu bidhaa au huduma. Hii inaweza kusababisha ongezeko la mauzo kwa wafanyabiashara.
Mifano ya Malipo Mdogo Mdogo
1. Duka la Mavazi: Mteja anaweza kununua nguo kwa malipo ya awamu tano ndani ya miezi miwili. Hii inamwezesha mteja kupata mavazi anayohitaji bila kuathiri bajeti yake ya kila siku.
2. Huduma za Kielektroniki: Huduma kama vile simu za mkononi au kompyuta zinaweza kulipiwa kwa awamu ndogo ndogo. Hii inasaidia wateja kupata bidhaa ghali zaidi bila kulazimika kutoa kiasi kikubwa cha fedha mara moja.
Jinsi Nemobase Inavyosaidia
Kupitia Nemobase, wafanyabiashara wanaweza kurekodi mauzo na kuweka malipo mdogo mdogo kwa urahisi. Hii ina faida zifuatazo:
1. Utunzaji Bora wa Taarifa: Nemobase inaruhusu wafanyabiashara kutunza taarifa za wateja na malipo yao mdogo mdogo. Hii inasaidia kufuatilia maendeleo ya malipo na kuhakikisha hakuna malipo yanayopotea.
2. Ufuatiliaji wa Malipo: Wafanyabiashara wanaweza kuona historia ya malipo ya kila mteja, hivyo ni rahisi kufuatilia malipo yaliyokamilika na yale ambayo bado yapo njiani.
3. Kuboresha Mahusiano na Wateja: Kwa kuwa na rekodi sahihi za malipo mdogo mdogo, wafanyabiashara wanaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wao. Wateja wanapopata huduma nzuri, wana uwezekano mkubwa wa kurudi tena na tena.
Jinsi ya Kurekodi Mauzo Kupitia Nemobase.
Wafanyabiashara wanaweza kurekodi mauzo yanayolipiwa mdogo mdogo kupitia mfumo wa Nemobase kwa kufuata hatua hizi:
1. Ingia kwenye app ya Nemobase.
2. Ongeza bidhaa zako.
3. Nenda kwenye kuongeza mauzo.
4. Ingiza jina la mteja na namba yake.
5. Ingiza bidhaa anayotaka kununua mdogo mdogo.
6. Kisha fuata maelekezo zaidi kupitia video hii:
https://youtu.be/grwWYRa5gg0?si=z9Iv5jMBa82a2Mpq
Kwa kutumia Nemobase, wafanyabiashara wanaweza kuongeza ufanisi wa biashara zao na kuboresha uzoefu wa wateja wao kupitia mfumo wa malipo mdogo mdogo. Hii inawasaidia kuongeza mauzo na kujenga uaminifu miongoni mwa wateja wao.
Pakua app ya nemobase kupitia link hii leo, na tumia bila malipo.
#Nemobase #MalipoMdogoMdogo #Biashara #Mauzo #HudumaBora #Fedha #HudumaZaKifedha